Jumanne 7 Julai 2026 - 12:10
Mamilioni ya Wairaq Wajiandaa Kumpokea Kiongozi Shahidi, Imam Khamenei, huko Najaf na Karbala

Hawza/ Kadiri muda wa mazishi ya mwili wa Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, nchini Iraq uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano unavyokaribia, ndivyo maandalizi ya kiutawala na kiufundi ya kuhakikisha kufanikiwa kwa tukio hili muhimu la kihistoria yanavyozidi kushika kasi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kadiri muda wa mazishi ya mwili wa Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, nchini Iraq uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano unavyokaribia, ndivyo maandalizi ya kiutawala na kiufundi ya kuhakikisha kufanikiwa kwa tukio hili muhimu la kihistoria yanavyoongezeka. Wakati huo huo, shauku kubwa imeonekana miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo, kiasi kwamba inatarajiwa zaidi ya watu milioni tano watashiriki katika mazishi hayo katika mikoa ya Najaf al-Ashraf na Karbala al-Mualla.

Maandalizi ya Kimuundo na Kiutendaji

Kwa ajili ya kuandaa tukio hili ipasavyo, imeundwa kamati ya ngazi ya juu inayojumuisha taasisi mbalimbali, zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Shirika la Hashd al-Shaabi, tawala za mikoa ya Najaf al-Ashraf na Karbala al-Mualla, Haram Takatifu za Alawi, Husseini na Abbasi, Wizara za Mambo ya Ndani na Uchukuzi pamoja na taasisi nyingine za serikali.

Katika muktadha huo, msemaji rasmi wa Kamati ya Habari ya Mazishi ya Imam Shahidi Khamenei, Luteni Jenerali Saad Maan, alisema katika mkutano mpana na waandishi wa habari kwamba; siku ya Jumanne kutafanyika hafla rasmi ya kuupokea mwili wa Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei, kwa ushiriki wa viongozi wa ngazi za juu wa serikali na wa dini kutoka Iran na Iraq. Aidha, kutafanyika maandamano makubwa ya wananchi siku ya Jumatano tarehe 17 Tir (July 7 2026) kuanzia saa 12:00 alfajiri.

Aliongeza kuwa njia ya maandamano katika Najaf al-Ashraf itaanzia Daraja la Kufa kuelekea Daraja la Thawrat al-Ishrin, kisha hadi Uwanja wa al-Sadrayn, ili wananchi washiriki katika mazishi na kumuaga kwa mara ya mwisho.

Ndani ya Karbala al-Mualla, maandamano yataanzia katika makutano ya Sayyid Joudah, kisha kupitia Barabara ya Gavana kuelekea Haram ya Imam Hussein (as), na baadaye kuelekea Haram ya Hadhrat Abul-Fadhl al-Abbas (as).

Saad Maan alieleza kuwa; mpango kamili wa usalama umeandaliwa kwa ushirikiano wa wizara, taasisi pamoja na vyombo vya usalama na huduma ili kuhakikisha washiriki wote wanapatiwa huduma zinazohitajika.

Pia aliwataka wananchi, vikundi vya kidini, mawakibu za Husseini na makundi yote yatakayoshiriki kufuata kikamilifu maelekezo ya kiusalama na ya uendeshaji yatakayotolewa hatua kwa hatua na mamlaka husika.

Likizo Rasmi katika Mikoa ya Iraq

Sambamba na hilo, serikali za mitaa za baadhi ya mikoa ya Iraq, ikiwemo Dhi Qar, Wasit, Karbala, Najaf al-Ashraf, Basra na Baghdad, zimeamua kutangaza siku ya Jumatano kuwa likizo rasmi ili wananchi wapate fursa ya kushiriki katika mazishi hayo.

Inatarajiwa kwamba serikali za mikoa mingine pia zitachukua hatua kama hiyo. Wakati huo huo, duru za wabunge na makundi ya kijamii zimeiomba Serikali ya Iraq kuitangaza siku ya Jumatano kuwa likizo rasmi ya kitaifa.

Ushiriki Mpana wa Makabila

Mbali na hayo, makabila mbalimbali ya Iraq katika maeneo ya kusini, Ukanda wa Furati ya Kati na maeneo ya kati ya nchi yametangaza utayari wake wa kushiriki kikamilifu katika mazishi hayo.

Masheikh wengi na viongozi wa makabila wamewataka vijana wao kuelekea Najaf na Karbala siku ya Jumanne ili kutoa heshima kwa Shahidi Imam Khamenei, ambaye daima alikuwa na misimamo ya heshima na utukufu kuhusu Iraq na wananchi wake, na hivyo kuweka kumbukumbu ya kudumu ya msimamo wao.

Sambamba na hilo, makumi ya mawakibu na vikundi vya Husseini vimeanza maandalizi ya kutoa huduma mbalimbali, zikiwemo chakula, vinywaji na sehemu za mapumziko kwa umati mkubwa wa washiriki.

Ushiriki Mkubwa wa Wasomi na Viongozi

Wakati ujumbe rasmi wa ngazi za juu pamoja na ujumbe wa kisiasa, kidini, kijamii na kitamaduni uliposhiriki katika mazishi yaliyofanyika Tehran, mamia ya viongozi wa serikali, wanasiasa, wanazuoni wa dini, viongozi wa makabila na wasomi wa vyuo vikuu wanatarajiwa kushiriki katika mazishi yatakayofanyika Najaf al-Ashraf na Karbala al-Mualla.

Miongoni mwao watakuwa mawaziri, viongozi wa vyama vya siasa, magavana, wanazuoni, maprofesa wa vyuo vikuu, masheikh wa makabila, wanafunzi wa vyuo vya dini na wanafunzi wa vyuo vikuu, wanawake na wanaume.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha